Home Habari STARS KUFA NA KUPONA SAUZI

STARS KUFA NA KUPONA SAUZI

410
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

BAADA ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali michuano ya COSAFA, leo vijana hao watatinga tena uwanjani kutafuta nafasi ya kuingia nusu fainali watakapovaana na wenyeji, timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.

Akizungumza na DIMBA kwa njia ya simu kutoka Afrika Kusini, kocha mkuu wa Stars, Salum Mayanga, alisema vijana wake wapo tayari kwa mapambano na ana uhakika leo wataibuka na ushindi.

“Kwanza niwapongeze vijana wangu kwa kazi nzuri waliyoionyesha mpaka kufika hatua hii, naamini hata mchezo wetu dhidi ya wenyeji wetu tunaweza kabisa kushinda na kutinga nusu fainali,” alisema.

Alisema amewanoa vijana wake kisawasawa na kilichobakia ni hizo dakika 90 ndani ya uwanja, huku akiwataka Watanzania kuiombea timu yao iweze kutwaa ubingwa huo.

Stars imefikia hatua hiyo baada ya kukusanya jumla ya pointi tano na mabao matatu kwenye kundi lao A lililokuwa na timu za Angola, Malawi na Mauritius.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here