SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

STRAIKA wa Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Jacksoni Muleka, amesema anatambua ubora wa Klabu ya Simba, lakini hana mpango wowote wa kujiunga nayo kutoka na dili kubwa alizonazo kutoka barani ulaya

Muleka ndiye kinara wa mabao wa Ligi ya DR Congo,Simba wanaisaka saini yake kwa udi na uvumba ili kuja kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inashikiliwa na Meddie Kagere kutoka Rwanda na John Bocco.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,kutoka Kishansa, Muleka alisema, anatamani sana kucheza Simba, lakini tayari anahitajika na timu kutoka Ubelgiji pamoja na Afrika Kusini ambazo zimefikia dau ambalo Klabu pamoja na Meneja wake wameliafiki.

Alisema,bado ana mkataba mrefu na TP Mazembe hivyo timu ambayo itamuhitaji lazima ijipange kikamilifu, ili kukidhi vigezo na masharti ya timu.

Unajua mchezaji ambaye yupo huru ana tofauti na yule mwenye mkataba, mimi niko chini ya Mazembe, nao lazima wapate faida yangu, walinisajili kwa pesa nyingi, hivyo lazima watahitahi pesa nyingi kuniuza ili gharama yao irudi.

Simba ni timu nzuri, hakuna mchezaji toka Congo anaweza kuikataa Simba, hata mimi siwezi kukataaa kama wataweza hilo dau waje niko tayari,îalisema Muleka.

Hata hivyo nyota huyo alisema, kutokana na janga hatari la maambukizi ya virusi vya Corrona , kwa sasa anajinoa nyumbani kwakwe kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here