SHARE

STRAIKA wa kimataifa wa Yanga, Mrundi Amis Tambwe, amesema ametimiza nadhiri yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa lazima aifunge Simba japo bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tambwe ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Simba, alifunga bao moja kati ya mawili ambayo Yanga ilishinda katika mch- ezo wa jana dhidi ya Simba.

“Nimefanikiwa kutimiza nadhiri yangu ya kuifunga Simba katika mchezo wa leo (jana), naamini sasa bado ninayo nadhiri nyingine ya kuhakikisha napata tuzo ya mfungaji bora wa msimu huu wa ligi,” alisema nyota huyo ambaye pia yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burundi.

Katika mchezo huo Simba walikuwa we- nyeji huku bao la pili la Yanga likifungwa na Malimi Busungu ambaye alitokea benchi ku- chukua nafasi ya Simon Msuva.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here