Home Habari TARIMBA KIULAINI KUMRITHI MANJI

TARIMBA KIULAINI KUMRITHI MANJI

4349
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE


WAKATI Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) ikitangaza kuwa fomu za uchaguzi wa Yanga zinaanza kutolewa kesho, jina la Tarimba Abass ndilo linalopigiwa debe kurithi mikoba ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ndiyo iliyobeba jukumu la kusimamia uchaguzi huo, na sasa imesema zoezi la kuchukua fomu linaanza rasmi kesho kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema Januari 13 mwakani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT), na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Malangwe Mchunguhela, kesho mchakato wa kuchukua fomu kwa wagombea unaanza, ambapo utamalizika Novemba 13.
Baada ya taarifa hiyo kutoka TFF, jina la Tarimba limekuwa likitajwa sana kwamba ndiye mwenye sifa za kuvaa viatu vya Manji, kwani anaijua Klabu hiyo nje ndani kutokana na kuiongoza miaka kadhaa iliyopita.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here