Home Habari TATIZO YANGA NI KOCHA AU WACHEZAJI?

TATIZO YANGA NI KOCHA AU WACHEZAJI?

1416
0
SHARE

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wamekuwa hawapati matokeo mazuri katika mechi za Ligi Kuu hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka huu.

Yanga wameonekana wakianza Ligi hiyo kwa kusuasua, ambapo katika mechi nne walizocheza wameshinda mechi mbili na kutoka sare michezo mitatu na kuwa katika nafasi ya sita na pointi tisa.

Katika mechi zake, Yanga imekuwa na tatizo kwenye safu ya ushambuliaji, ambayo inaonekana kuwasumbua na kushindwa kupata matokeo mazuri.

Kutokana na hali hiyo, wadau wa soka nchini na mashabiki wa Yanga wamekuwa wakihoji juu ya tatizo hasa linalosababisha timu hiyo kushindwa kufanya vema kwa sasa.

Mwishoni mwa wiki hii Yanga walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kutoka sare ya bila kufungana, huku wakionekana kuendelea kuandamwa na zimwi la kushindwa kufanya vema.

Bado mashabiki wa Yanga wameendelea kulalamikia matokeo hayo na kuhoji tatizo hasa kwenye timu hiyo, ni wachezaji au kocha?

Ukiwa kama mdau wa soka nchini na mfuatiliaji mzuri wa michuano ya Ligi hiyo, unazungumziaje suala hilo?

Toa maoni yako ukianzia na jina kamili na mahala ulipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here