Home Michezo Afrika TOURE ATOA NENO KOMBE LA DUNIA

TOURE ATOA NENO KOMBE LA DUNIA

4591
0
SHARE
CAPE TOWN, Afrika Kusini

MCHEZAJI wa zamani wa Ivory Coast, Kolo Toure, amewapa neno timu zinazoshiriki Kombe la Dunia hasa za kutoka Afrika kwa kusema kwamba kuna kila sababu ya kubadilisha mtazamo kwa kujituma zaidi.

Akisema kwamba, jambo kubwa kwenye soka la Afrika ni kuongeza juhudi kwenye fainali za mwaka huu kutokana na umuhimu wa michuano ya mwaka huu hasa kwa sababu Afrika ina vikosi bora ikilinganishwa na baadhi ya timu za kutoka mabara mengine.

Alisema kwamba, moja ya timu bora ambayo anaamini haitakuwa na uwakilishi wa wasiwasi ni Misri pamoja na Nigeria ambazo nimeonyesha kuwa na jambo la ziada kutokana na wachezaji wao mmoja mmoja katika kila timu.

“Kimsingi kuna mambo ambayo Waafrika wanatakiwa kuyaangalia kwa macho mawili wakati wanaelekea Kombe la Dunia msimu huu. Tumeona kuna mabadiliko makubwa kwa timu nyingi lakini niseme wazi kwamba kwa timu zilizopo kwenye fainali ya mwaka huu, Afrika tutakuwa na uwakilishi mzuri sana.

“Nimeona timu kama Misri, Nigeria ni moja ya vikosi bora sana kwa sasa. Kuna wachezaji bora ambao wanaweza kuamua matokeo wakati wowote.

“Imani yangu huu utakuwa msimu bora wa Afrika kufanikiwa tofauti na wengi wanavyoitazama,” alisema Toure ambaye kwa sasa yupo kwenye dawati la ufundi la timu ya Taifa ya Ivory Coast maarufu kama Tembo.

Beki huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester City zote za England, ameshacheza mechi kadhaa kubwa ikiwemo fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 2010.

Pia Toure akiwa na Manchester City, aliweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) katika msimu wa mwaka 2012.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here