Home Habari TSHABALALA HATAISAHAU FAINALI YA FA

TSHABALALA HATAISAHAU FAINALI YA FA

645
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE

BEKI wa kushoto wa timu ya Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, amesema kuwa katika maisha yake hataisahau mechi ya Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Alisema mchezo huo umemrudisha nyuma malengo yake baada ya kuumia, kwani alikuwa na malengo mengi msimu huu lakini yote yamepotea kutokana na majeraha.

“Unajua nilikuwa na malengo yangu ya kuondoka na kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania na kuna watu walikuwa wananifuatilia na kama ningeenda kwenye michuano ya Cosafa iliyofanyika Afrika Kusini sidhani kama ningerudi.

“Maana kuna watu walikuwa wananifuatilia na kuna timu kadhaa zilikuwa zinanihitaji, lakini walikata tamaa baada ya mimi kuumia,” alisema Tshabalala.

Alisema kwa sasa anashukuru Mungu amepona na yupo fiti ila kocha wake Joseph Omog bado hajaamua kumtumia.

Tshabalala ni mmoja wa wachezaji walioichezea Simba mecho zote za msimu uliopita kabla ya kuumia kwenye mchezo wake wa mwisho wa fainali ya FA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here