SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

WAKATI Yanga inatarajia kuvaana na Kagera Sugar leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kiungo wa timu hiyo, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi ametimkia  kwao kuangalia familia yake.

 Akizungumza  na DIMBA  jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael, alisema Papy alimuaga siku moja kabla ya kuanza nao mazoezi, kuwa anamatatizo ya kifamilia hivyo  anasafiri kwenda kuwaona jamaa zake.

Hata hivyo alisema amempa siku chache kwa kuwa hajawahi kuwa pamoja nae mazoezini tangu ameanza, hivyo anatakiwa kuwahi ili apate muda wa kumsoma vizuri.

“Nimefuatilia baadhi ya viedo za Yanga, Papy ni mchezaji mzuri, lakini nahitaji awahi kurudi ili afanye mazoezi na wenzake kwani  tunakazi kubwa  ambayo inatukabili mbele yetu,”alisema Eymael.

Hata hivyo Tshishimbi alizungumza na DIMBA kutoka, DR Congo, na kusema  familia yake kwa sasa ipo salama, hivyo anatarajia kurudi kabbla ya mchezo wao dhidi ya Azam FC.

“Sikupanga kuja nyumbani kwa  kipindi hiki lakini amenilazimu kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezon wangu, lakini nitarudi haraka  sitaki kukosa mechi ya Azam, pia sijahudhuria maoezi na kocha wetu mpya tangu ameanza,”alisema Tshishimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here