Home Habari TSHISHIMBI ATOA YA MOYONI KUINUSURU YANGA

TSHISHIMBI ATOA YA MOYONI KUINUSURU YANGA

7828
0
SHARE

NA MWAMVITA MTANDA


KIUNGO wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, ameweka wazi kinachowakwamisha kwa sasa kuwa ni kutokana na baadhi ya wachezaji wenzake kukata tamaa mapema, lakini akawaambia mashabiki wao mambo mazuri yanakuja.

Tshishimbi ameliambia DIMBA Jumatano ikiwa ni siku chache baada ya kikosi cha Yanga kupokea kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Gor Mahia ya Kenya, mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Jumapili iliyopita Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Tshishimbi alisema wao kama wachezaji wanajua mashabiki wao wanaumia kutokana na matokeo mabaya yanayowaandama, lakini ana uhakika Ligi Kuu Bara itakapoanza watauwasha moto.

“Ni kweli mashabiki wetu wanaumia sana kutokana na matokeo mabaya tunayoyapata, lakini niseme tu nina uhakika hali hii haiwezi kujitokeza kwenye ligi, tutapambana vilivyo.

“Unajua wapo baadhi ya wachezaji wenzetu wanaonekana kama kukata tamaa lakini tunazidi kutiana moyo ili kuhakikisha timu yetu inarudi kwenye ubora wake,” alisema Tshishimbi.

Alisema kwa sasa kinachotakiwa ni umoja na mshikamano kwa Wanayanga wote, kwani ndicho ambacho kinaweza kuwasaidia kupata mafanikio akidai sehemu yoyote ambayo kuna malumbano mambo hayawezi kwenda vizuri.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here