SHARE

NA CLARA ALPHONCE

YANGA imewakata kilimilimi wale waliokuwa wakidhani Wanajangwani hao wameshindwana na kiungo wao, Kabamba Tshishimbi, kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha na sasa mkali huyo wa kucheza na dimba la kati anawasili kesho tayari kuanza kazi.

Taarifa zilizokuwa zimezagaa mitaani ni kwamba, kiungo huyo alikuwa hajamaliza mkataba wake na timu yake ya Mbabane ya nchini Swaziland, na kwamba Yanga wameshindwa kuvunja mkataba huo, lakini Wanajangwani hao wamejibu mapigo ambapo rasta huyo anatia maguu kesho.

Yanga waliingia mkataba wa awali na mchezaji huyo, lakini walishindwa kumtangaza kama wengine kwa kuwa ana mkataba na klabu yake ambao unakwisha mwezi ujao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here