Home Hadithi TSHISHIMBI NDANI YA NYUMBA PEMBA

TSHISHIMBI NDANI YA NYUMBA PEMBA

415
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa kwani yule kiungo rasta aliyesemekana ameyeyuka Yanga, Kabamba Tshishimbi, ametua rasmi kisiwani Pemba kwenye kambi na atauwasha moto dhidi ya Simba, katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga wamemalizana na kiungo huyu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), waliyemsajili kutoka Mbabane Swallows ya nchini Swaziland, ambapo alitua nchini juzi na jana akaunganisha kwenda Pemba, kujiunga na wenzake wanaojiandaa na mchezo huo dhidi ya Simba.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Dismas Ten, alilithibitishia DIMBA Jumatano kwamba, kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kumiliki sehemu ya katikati mwa uwanja, yupo tayari kwa mapambano.

“Tulishamalizana naye na leo (jana), atakwenda Pemba kujiunga na wenzake kambini kujiandaa na mchezo wetu wa Ngao ya Jamii (dhidi ya Simba), hiyo Agosti 23,” alisema.

Kiungo huyo anatarajiwa kuliziba vizuri pengo lililoachwa na Haruna Niyonzima aliyetimkia Simba, ambapo mashabiki wa Yanga wanaamini kwamba wamepata mtu wa kazi kutokana na kupitia rekodi zake huko alikokuwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here