SHARE

MWAMVITAMTANDA

MIAKA 10 ya kilele cha tamasha la SportPesa Simba Week au ikifahamika kwa miaka mingi kama Simba Day, un- aweza kusema jana lilifunika kuliko yote yaliyowahi kupita baada ya matukio mengi ya kuvutia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba iliendeza mfululizo wa mata- masha yake hayo tangu mwaka 2009, wakati klabu hiyo ilipokuwa chini ya mwenyekiti Hassan Dalali, ambapo sherehe hizo zilikuwa zikifanyika Agosti 8 kila mwaka, lakini mwaka huu lime- wahi mapema kutokana na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutoka mapema.

Safari hii ilikwa kama funga kazi, sherehe hizo zilianza Agosti 1, kwa mashabiki wa klabu hiyo pamoja na wa- nachama kufanya shuguli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu.

Juzi Jumatatu ndipo hasa sherehe hizo zilipowakuna mashabiki wake pale mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji ‘MO’, alipoambatana na mgeni rasmi Waziri wa Habari Utamaduni, Sa- naa na Michezo, Dkt. Harrison Mwaky- embe, kutembelea ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo uliyopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Saalam na kuweka jiwe la msingi.

Katika tukio hilo, MO aliwaahidi Wa- nasimba kuwa gharaza za matengenezo ya uwanja huo pamoja na miundombinu yake, hazitahusika na fedha za uwekez- aji wake wa asilimia 49, na badala yake atazitoa yeye mwenyewe binafsi.

Katika kilele cha maadhimisho ya siku hiyo jana, ndipo historia mpya ya kuujaza uwanja huo ilipotimia kwasaba- bu hadi inafika saa 11 jioni hakukuwa na nafasi uwanjani na hivyo kusababisha baadhi ya mashabiki kubaki nje.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Ma- wasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema umati uliohudhuria tamasha hilo ulizidi idadi ya kawaida ya watu 60,000 wanaotakiwa kuujaza uwanja huo.

Tukio hilo lililohudhuriwa na Wa- ziri Mkuu, Kassim Majaliwa, na viongozi mbalimbali wa Serikali, lilianza kwa burudani mbalimbali ikiwemo bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ iliyokuwa ikitumbuiza uwanjani hapo, kabla ya kuanza zoezi la kutambulisha wachezaji

Kazi ya kutambulisha wachezaji ili- fanywa na Manara aliyeingia uwanjani huku akisindikizwa na walinzi mida ya saa 10.56 jioni na kukabdhiwa kipaza sauti, na kisha kusalimia mashabiki kwa salamu maarufu ya klabu hiyo inayoitwa ‘This is Simba’.

Manara alianza kulitambulisha ben- chi la ufundi chini ya kocha mkuu, Patrick Aussems, na kisha kuanza na mche- zaji kijana ndani ya kikosi hicho, Rashid Juma.

Wachezaji waliofuata ni Ali Salim, Yusuf Mlipili, Muzamir Yassin, Said Ndemla, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Jonas Mkude, Kennedy Juma na Miraji Othman.

Wengine waliofuata ni Haruna Shamte, Hassan Dilunga, Shomari Ka- pombe, Aishi Manula, Pascal Wawa, Hendirick Da Silva, Tairone Da Silva, Gerson Fraga na kipa aliyekipiga Yanga msimu uliopita, Benno Kakolanya.

Wachezaji wengi waliotambulish- wa katika kikosi hicho ni Deo Kanda, Clatous Chama, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Sharaf Shibob, Francis Kahata, Erasto Nyoni, John Boc- co aliyekua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na Ibrahim Ajib Migomba.

Baada ya mashabiki kushangilia kwa nguvu zote, Manara alitangaza kumwita mchezaji mwingine akimtambulisha ku- cheza nafasi mbalimbali kama golikipa, beki, kiungo na straika, kisha kumuita uwanjani MO Dewji. Jina la Mo Dewji liliamsha shangwe kutoka kila kona ya uwanja huo.

Baada ya tukio hilo likifuatwa na wanachama na wapenzi mbalimbali ku- toa salamu zao, timu hiyo ikiwa na sura mpya, ilijitupa uwanjani kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Kagere aliibuka shujaa akifunga mabao matatu Simba ikishinda 3-1 na kupandisha mzuka wa kuelekea mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika wikendi hii dhidi ya US do Songo ya Msumbiji.

Makali ya Simba yalianza kuoneka- na mapema tu mara baada ya kipenga cha Donisya Rukya kupulizwa kuashiria kuanza kwa mchezo huo.

Kagere alipachika bao hilo kufuatia uzembe wa kipa Lawarence Mulenga ali- yeshindwa kucheza mpira uliorudishwa kwake.

Simba kuendelea kulisakama lango la wapinzani wao ambapo dakika ya 15 almanusura wapate bao la pili kupi- tia kiungo wao wa kimataifa Clatous Chama aliyechonga kona lakini mpira ukapaa juu ya lango la Power Dynamos.

Dakika ya 21, Chama alikosa bao baada ya shuti lake kudakwa kabla da- kika ya 22 Mzamiru Yassin kukosa goli la wazi akishindwa kutumia vyema pasi kutoka kwa Francis Kahata lakini mpira ukawahiwa nana beki wa Power Dyana- mos.

Wazambia hao walijibu masham- bulizi hayo kwa nguvu dakika ya 24 na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia Jimmy Dlingai akiunganisha vy- ema mpira wa kona kwa kichwa na ku- muacha kipa Beno Kakolanya akiduwaa.

Simba iliendeleza mashambulizi da- kika 38 kupitia kwa Tshabalala aliyepora mpira kutoka kwa mabeki wa Power Dy- namos na kumpa pasi Deo Kanda lakini ukaokolewa na kuwa kona ambayo hai- kuzaa matunda.

Dakika ya 35, Mbrazil Santos Da Sil- va aligongeana pasi nzuri na Deo Kanda na kumpa Kapombe lakini shuti lake likapaa nje ya lango la Dynamo ambapo timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku Simba wakiliandama zaidi lango la wapinzani wao.

Hadi mapumziko timu hizo zilik- wenda kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo kipindi cha pili mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara walirudi na moto ambapo dakika ya 59, Kagere alipachika bao la pili baada ya kupokea pasi ya Kanda.

Dakika ya 73, Kagere akawainua tena mashabiki wa Simba kwa bao la tatu ambalo likampa ‘ hat trick’ baada kuuanganisha mpira wa kona ulio- chongwa na Chama na kutumia guu lake la kulia kuujaza wavuni.

Kikosi cha Simba: Beno Kakolanya,Shomary Kapombe, Tairon Santos da Silva,Pascal Wawa, Mzamiru Yasin, Deogratus Kanda, Sharaf Eldin Shabib, Meddie Kagere, Claotus Chama na Francis Kahata.

Power Dynamos: Laurence Mu- lenga, Larry Bwalya, Raphael Maku- buli, Simmy Dlingai, John Solo, White Mwambaba,Benson Sakala,Kondani Chiboni, Christian Mtoba,Fedrick Mu- lamba na Kassim Titus.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here