SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya ukimya wa muda mrefu, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shabaan ‘Keisha’, yuko mbioni kurudi upya kwenye gemu baada kupotea kwa muda mrefu kutokana na kubanwa na majukumu ya shule na ulezi.

Keisha ameliambia DIMBA Jumatano kwamba tayari ameshaingia studio kukamilisha kitu chake kipya ambacho anatarajia kukiachia hewani siku za hivi karibuni akiamini itamrudisha kwenye ubora wake.

“Bado nipo kwenye muziki kwa kuwa ndio kazi yangu, nakaribia kuachia ngoma yangu mpya ambayo ipo jikoni na wakati wowote itakuwa sokoni, mimi sifanyi muziki wa kiki kwa kuwa siamini katika hilo, natambua uwezo wangu hivyo najipanga mimi mwenyewe na simtegemei mtu katika kutoa nyimbo kwa kuwa najiamini,” alisema Keisha.

Keisha ambaye ni mama wa watoto wawili, pia amehitimu shahada ya ununuzi na ugavi katika Chuo Kikuu cha Biashara (CBE).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here