Home Uchambuzi MAAJABU YA ASALI NA MDALASINI-2

MAAJABU YA ASALI NA MDALASINI-2

1046
0
SHARE

Na Grace Shitundu

Wiki hii katika kona hii ya Afya, tunaendelea kuangalia maajabu ya asali na mdalasini.

Asali husaidia kuirudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu kama dondola na washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni zilizofanyika nchini Australia na Japani, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani kwa kutumia kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi.

Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji, kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi na kisha kunywa tena alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka.

Asali ina uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi, halafu osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

Kusukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis) kutokana na uwezo wa asali kuua bakteria.

Matumizi ya kila siku ya asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi wawapo mkutanoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here