Home Chombezo UKIWA HIVI MWANAMKE HABANDUKI KWAKO! – 2

UKIWA HIVI MWANAMKE HABANDUKI KWAKO! – 2

616
0
SHARE

NA JOSEPH SHALUWA, 0712 170 745

USISHANGAE kuwaona akina fulani wanadumu kwenye uhusiano wao kwa muda mrefu, huku kwa upande wako mambo yakiharibika. Usije kujiuliza ni vipi kwao tu, kwako mambo hovyo?

Ni kwamba wenzako wanawekeza kwenye uhusiano, wakati wewe ukienda
ilimradi siku zinakwenda. Kwa hakika hamuwezi kuwa sawa.

Ndiyo sababu tunajifunza somo hili. Ni mada iliyoanza wiki iliyopita
na leo tunamalizia sehemu ya mwisho. Tunaangalia ni mambo gani
wanawake wanavutiwa zaidi kwa wanaume. Au niseme vitu gani ukivifanya kwa mwanamke wako hatafikiria kukuacha.

Tuendelee na mada yetu.

KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana
kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda
kuwasifia wanaume zao.

Kumsifia mwanamke kuna nafasi kubwa sana kwake. Jenga utamaduni wa
kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo.

Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na
unamfanya azidi kukupenda, kwa kuwa anaamini yupo na mwanamume ambaye
anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake
katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati
mwingine ikilazimika kumwambia mwenzi wake basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.

Hii si sahihi. Mwenzako anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako
nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza
kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi
ya kujiona mwanamke kamili katika penzi lenu.

MPE KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia.
Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama
nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea akawa katika hali hiyo,
msikilize.

Mathalani, ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake
anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu,
kutampa matumani kwamba yupo na mtu sahihi.

Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo. Msikilize, mshauri
panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande
wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au
kifamilia, mshirikishe.

Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako,
kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema.
Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa
mwanamke.

TENDO LA NDOA

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki
kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha
ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na
kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na
kutengewa muda maalumu wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya
wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha
zaidi wenzao. Wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya
kuwakomoa wenzao.

Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya
maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza
kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo
wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini
nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?

Kuna kitu nimesahau? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe
kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja;
uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako.

Jiandae kupata kitabu changu kipya cha SIRI ZA MAISHA YA NDOA YENYE
FURAHA, kitakachokuwa mitaani hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here