Home Habari ULINZI WAIMARISHWA KILA KONA

ULINZI WAIMARISHWA KILA KONA

649
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

HALI ya ulinzi wa Uwanja Taifa jana ilikuwa imeimarishwa kila pembe kwa kikosi cha Jeshi la Polisi kujipanga kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

DIMBA, ambalo lilikuwa limepiga kambi tangu asubuhi kabla ya mageti ya uwanja huo kufunguliwa ili kuruhusu mashabiki kuingia, lilishuhudia askari wa vikosi vya farasi na mbwa wakifanya mazoezi kujiweka sawa kwa ajili ya kuimarisha doria.

Aidha, magari ya kubeba maji ya kuwasha yalionekana kusambazwa maeneo ya uwanja huo kama sehemu ya kujiweka tayari kwa lolote linaloweza kutokea.

Licha ya ulinzi huo wa kuonekana, pia Jeshi hilo lilimwaga mashushushu wa kutosha ambao walikuwa wakirandaranda kunusa harufu ya uhalifu wa aina yoyote ambao ungeweza kujitokeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here