SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA Gift Starnford au Gigy Money amefunguka jinsi anavyotumia muda wake vyema kusaka pesa kwa kuwa anaogopa sana wanaume wanaowategemea wanawake kuwaweka mjini.
Gigy ambaye ni mama wa mtoto mmoja amesema mara nyingi watu wanadhani yeye ni mtu wa starehe sana lakini ukweli ni kwamba amekua akipigana usiku na mchana kutafuta pesa ili aweze kujitegemea na si kumtegemea mwanaume.
Akizungumza na DIMBA Jumatano,Gigy alisema, anaumiza akili sana kujua jinsi ya kupata pesa na ndio maana kwa sasa amekua akipata michongo mingi ikiwemo kuwa balozi wa bidhaa mbalimbali, jambo ambalo anamshukuru sana Mungu.
“Naumiza sana akili kupata pesa, nipo tayari kukesha klabu au sehemu zozote za starehe, ili nipate pesa,hawa wanaume wanaotegemea wanawake siwaleaji kabisa, na siwezi kuwa na mtu kama huyo na ndio maana siyumbishwi na maisha”alisema Gigy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here