Home Habari UWANJA WA TAIFA WAFUNGULIWA RASMI

UWANJA WA TAIFA WAFUNGULIWA RASMI

1160
0
SHARE

NA SALMA MPELI

UWANJA mkuu wa Taifa ambao ulikuwa katika matengenezo kwa takribani miezi mitatu, sasa umefunguliwa na unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia Novemba 24, mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa uwanja huo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe, alisema kuwa, uwanja ni mzuri na sasa unaonekana kukamilika, kwani hata vile vipara vilivyokuwa vinaonekana awali vimepotea.

Mwakyembe alisema, Serikali itakabidhiwa uwanja huo rasmi na Kampuni ya mchezo ya kubahatisha ya SportPesa ndani ya siku kumi na hivyo kuiomba TFF kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi, kupanga mechi moja ichezwe katika zoezi la uzinduzi na makabidhiano ya uwanja huo.

“Uwanja umekamilika na leo nimeukagua na kuridhishwa na ukarabati mkubwa uliofanywa, wameniambia baada ya siku 10 utakuwa tayari, hivyo nimewaomba TFF kuangalia uwezekano wa kutafuta japo mechi moja ichezwe wakati wa ufunguzi Novemba 24,” alisema Mwakyembe.

Aliongeza kuwa, wapo vijana sita ambao wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa Uwanja, hivyo ameomba kuangaliwa kwa ajira zao ili waweze kutumika katika viwanja vingine vya mikoani.

Mwakyembe alisema, kubwa linalotakiwa kwa sasa ni Watanzania kwa ujumla kushirikiana katika kuutunza uwanja huo, kwani gharama kubwa zimetumika katika ukarabati wake, ambazo awali zilitajwa ni Sh bilioni 1.2, lakini ukimalizika kabisa ndiyo watajua gharama zote zilizotumika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here