Home Burudani UWOYA ACHOTA MILIONI 25 KWA DOGO JANJA

UWOYA ACHOTA MILIONI 25 KWA DOGO JANJA

7989
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE            |    


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abdulaziz Chande au Dogo Janja, amesema tayari ameridhia kumlipa Sh milioni 25 anachotaka mke wake, Irene Uwoya, ili aweze kucheza kwenye wimbo wake kama video Queen.

Irene Uwoya aliwahi kuripotiwa kuwa hapendi kushirikishwa kwenye video za Bongofleva, lakini kwa mume wake atafanya hivyo endapo atakuwa tayari kumlipa kiasi kisichopungua Sh milioni 25.

Akizungumza na DIMBA, Dogo Janja alisema, ameona ni wakati wa kumtumia zaidi Uwoya kwa kuwa ana vigezo vyote, badala ya kutumia pesa nyingi kwa warembo wengine.

“Nilizungumza naye ameonyesha utayari, nashukuru  na nitakuwa tayari kumlipa hiyo pesa…najua zinarudi nyumbani…ni mwanamke mwenye vigezo vyote, hivyo sitasita kumshirikisha pale ninapomhitaji,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here