Home Burudani VAN DIJK: NIACHIENI RONALDO J’MOSI

VAN DIJK: NIACHIENI RONALDO J’MOSI

8640
0
SHARE

MERSEYSIDE, England


 

BEKI kisiki wa Liverpool, Virgil van Dijk, amewatoa hofu mashabiki wa Liverpool wanaomuota Cristiano Ronaldo kuelekea mtanange wa fainali, akiwaambia wasiwaze, kwani ‘atadili’ naye.

Liver na mabingwa hao watetezi, Madrid, watamalizana Jumamosi ya wiki hii, mchezo utakaochezwa mjini Kiev, Ukraine, ambao utaamua litakakokwenda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha LFCTV, Mholanzi huyo alisema atatembea na Ronaldo kwa dakika zote 90 au zaidi za mechi hiyo.

“(Ronaldo) amekuwa akifunga mabao mengi kwa miaka michache iliyopita na hakuna ubishi kuwa ni mtu hatari.

“Lakini natakiwa kutembea naye kama timu yangu itakavyokuwa ikienda sambamba na wachezaji wengine wenye ubora,” alisema beki huyo wa kati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here