Home Burudani Vanessa aonyesha mahaba yake kwa Chriss Brown

Vanessa aonyesha mahaba yake kwa Chriss Brown

0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA anayefanya vyema kwenye kiwanda cha muziki hapa Bongo, Vanessa Mdee ametoa ya moyoni na kudai ni namna gani anamkubali mwanamuziki wa nchini Marekani Chriss Brown.

Vanessa anefunguka baada ya staa huyo wa Marekani kumfollow kupitia mtandao wa Instagram na kuwa miongoni mwa mastaa wachache kufuatiliwa na staa huyo mkubwa duniani.

ìNaamini wote mnatambua kuwa nimekua nikimfatilia Chriss Brown kwa ukaribu mkubwa, na ninapenda ufanyaji wake wa kazi, ni mtu ambaye nimekua nikimfatilia tangu naanza muziki hadi sasa, namkubali sanaîalisema Vanessa.

Aidhaa kitendo hicho kimetafsiriwa huenda staa huyo amevutiwa na kazi za Vanessa na baada ya kutangaza ujio wa kazi yake na Davido wa Nigeria huenda mwanadada huyo akawa miongoni mwa mastaa watakaofanya naye kazi hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here