Home Burudani VANESSA: NINA MIPANGO MINGI NA NYOVEST

VANESSA: NINA MIPANGO MINGI NA NYOVEST

596
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee, amezidi kuonyesha uwezo wake baada ya kutokea kwenye ngoma ya Rapa Cassper Nyovest wa Afrika Kusini, inayokwenda kwa jina la ‘Baby Girl’ huku akisisitiza ana mipango endelevu na rapa huyo.

Vanessa ameonekana kwenye ngoma hiyo kama ‘video queen’ na kudai wapo kwenye mipango ya kuja kufanya kazi pamoja katika siku za hivi karibuni.

“Tuna mipango endelevu na Cassper Nyovest, nimeonekana kwenye video na sasa nipo kwenye mipango ya kufanya naye ngoma moja, watu wangu wasubirie kidogo kuna mambo mazuri yanakuja hivi karibuni,” alisema Vanessa ambaye kwa sasa yupo kwenye tamasha la Fiesta mikoani.

Aliongeza kuwa kwa sasa kazi yake ni kuhakikisha anazidi kujitangaza kimataifa na kuutangaza muziki wa Kitanzania hivyo mipango yake ya kufanya kazi na wasanii wakubwa ni mingi na ataifanyia kazi kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here