Home Burudani VANESSA: SINA HARAKA NA UZAZI

VANESSA: SINA HARAKA NA UZAZI

787
0
SHARE

NA KYALAA SEHEYE,

STAA wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ‘V- money’, amesema suala la kuzaa ni muhimu kwa mwanamke lakini kwake kwanza anatamani kupambana na maisha na baadaye Mungu akipenda atatafuta mtoto.

Vanessa aliliambia DIMBA kuwa binafsi anachukua maamuzi hayo kutokana na ukweli kwamba maisha magumu na pia mchango wake unahitajika sana ili kusaidia jamii inayomzunguka wakiwamo ndugu zake.

“Bado ninalea watoto wa ndugu zangu nikiangalia bei za vitu vingi bado viko juu nasubiri  wakue kwanza na mimi ndio nizae kwa kuwa tukizaa wote kwa wakati mmoja tutashindwa kuwalea watoto,” alisema Vanessa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here