SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

KIKOSI cha Kagera Sugar na Azam FC kikae tayari, kwani Video zao  tayari zipo mikonini mwa Mbelgigi wa Yanga, na ameshamsoma kila mchezaji

KWELI Yanga sasa wamejiandaa kutimiza ndoto yao ya kutwaa ubingwa msimu huu, kwani baada ya kushusha kocha mpya na majembe ya akutosha sasa wanafanya umafia dhidi ya timu wanazokutana nazo Ligi kuu.

Tayari kocha Mkuu amesdhaagiza na kuzitia mkononi video za timu za Azam FC na Mtibbwa Sugar zitakazocheza nao mechi zinazofuata.

Yanga na Kagera Sugar, zitaumana leo katika Uwanja wa Taifa. Dar es Salaam na baada  ya siku chache Wanajangwani  hao wataivaa Azam FC.

Akizungumza na DIMBA jana, kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema, kabla ya kutua Yanga alishaanza kuzifuatilia timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara katika mitandao ya kijamii, lakini pia juzi alikabidhia video ya Kagera Sugar na Azam kwa kuwa ndio mechi  zinazokuja mbele yao.

Alisema anafahamu kila timu inahitaji matokeo mazuri, lakini kwa upande wake amejipanga  kupata ushindi wa pointi na mabao zaidi ili kupanda kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini nay eye anahitaji nafasi hiyo. “Kila timu ina ubora wake lakini naweza kusema yangu ni bora zaidi, kwa namna ambavyo nimepitia video tayari nimeshafahamu mbinu zao na upambanaji wao hivyo nitajua namna ya kuwamaliza uwanjani,”alisema Eymael

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here