Home Habari VIFAA VIPYA SIMBA HADHARANI JUMANNE

VIFAA VIPYA SIMBA HADHARANI JUMANNE

524
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE,

MABINGWA wa Kombe la FA, Simba wanatarajia kuingia kambini rasmi Jumanne, mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day, Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Mjumbe wa Kamati ya Wanachama ya Simba, Shaban Nyaa, alisema uongozi wa Simba umempa taarifa ya kufanya maandalizi na kuipokea timu Jumanne, ambapo wataweka kambi hapo kwa wiki mbili kabla ya kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kambi nyingine.

“Hapa watakaa kama wiki mbili kwa ajili ya mazoezi mepesi, huku wakiwa wanasubiri wachezaji wote wawasili na hapo ndipo wataondoka kwa ajili ya kambi nyingine Afrika Kusini,” alisema Nyaa.

Hata hivyo, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Iddy Kajua, alisema timu hiyo itakuwa Morogoro kwa muda huku wakiendelea na mipango ya kuipeleka kambi nje ya nchi.

Wachezaji ambao watakuwa kivutio kwenye kambi hiyo ni pamoja na Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Aishi Manula, Shomary Kapombe na John Bocco ambao ni wapya msimu huu kwenye kikosi cha Simba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here