Home Habari Vigogo Simba wamfuata Okwi Denmark

Vigogo Simba wamfuata Okwi Denmark

1423
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

WAKATI Simba ikiendelea na kasi yake ya kuzifunga timu zinazowasogelea, taarifa njema kwa mashabiki wao ni kwamba, taratibu za kumrudisha nchini Emmanuel Okwi zinakwenda vizuri.

Okwi, ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Simba, anaichezea SonderjykE ya nchini Denmark, lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanafanya juhudi kubwa za kumrejesha ambapo hata mchezaji mwenyewe ameonyesha nia, jambo ambalo linawapa wepesi Simba.

Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa, kuna vigogo wawili wenye ushawishi mkubwa ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi wametumwa nchini Denmark kukutana na Okwi na waajiri wake.

Katika timu hiyo, Okwi amekuwa hapati namba, ndiyo maana naye ameona bora arejee kwenye timu yake na viongozi wa Simba wanafanya kila linalowezekana ili kukamilisha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine, wakati harakati hizo zikiendelea, taarifa nyingine zinadai kuwa, wanamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Kipre Tchetche, anayekipiga nchini Oman.

Kama dili hilo likitiki, Wekundu hao wakafanikiwa kumrejesha Okwi, pia wakainasa saini ya Kipre, Simba itakuwa moto wa kuotea mbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here