Home Habari VIGOGO WAIPA SIMBA KOMBE LA FA DODOMA

VIGOGO WAIPA SIMBA KOMBE LA FA DODOMA

463
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE,

KUELEKEA mechi ya fainali ya Kombe la FA wikiendi hii kati ya Simba na Mbao FC, mawaziri, wabunge, wanachama na vigogo wengine wa Wekundu hao wa Msimbazi, wapo katika mikakati mizito ya kuhakikisha timu hiyo inatwaa taji hilo.

Baadhi ya wabunge na wanachama wa klabu hiyo wakiongozwa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu, wamesema mchezo huo ni mgumu kwani Mbao si timu ya kuibeza kwa namna ilivyozitoa jasho baadhi ya timu ikiwemo mahasimu wao kisoka Yanga.

“Kinachotakiwa ni wachezaji wetu wajitume na wajue tuna uchungu wa kukosa kushiriki michuano ya kimataifa kwa misimu minne, kikubwa tunataka mabao ya mapema ili kuwamaliza Mbao mapema ndio maana tumeanza mikakati mizito,” alisema Zungu.

Katika hatua nyingine, vigogo hao kuelekea kwenye mchezo huo wamekubali kuwaandalia chakula cha usiku wachezaji 40 katika Hoteli ya Morena, iliyopo Dodoma Ijumaa na pia watapata muda wa kuongea nao na kuwaeleza umuhimu wa mchezo huo, ambao utawapa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana na Zungu, wameunda kamati maalumu ya kuratibu suala hilo iliyokuwa chini ya Maulid Mtulia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here