SHARE

LOS ANGELES, Marekani

MWIGIZAJI maarufu, Vin Diesel, ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia filamu ya Fast and Furious, ametajwa kuwa ndiye mwigizaji wa kiume anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani.

Kwa mujibu wa jarida la watu maarufu la Forbes, Vin Diesel, amempiku mwigizaji mwenzake ambaye alikuwa akiongoza kwa kulipwa fedha nyingi, Dwayne ‘The Rock’ Johnson, ambaye kwa sasa analipwa dola 1.5 bilioni wakati Vin Diesel analipwa dola bilioni 1.6.

Chati ya malipo ya waigizaji inaonyesha kuwa Vin Diesel anaongoza kwa kulipwa dola bilioni 1.6, akifuatiwa na Dwayne Johnson (dola bilioni 1.5), huku Gal Gadot, akilipwa dola bilioni 1.4.

Emma Watson yeye anachukua dola bilioni 1.3, Johnny Depp (dola bilioni 1.1), Daisy Ridley (dola bilioni 1.08), Tom Holland (dola milioni 888), Chris Pratt (dola milioni 864), Chris Hemsworth (dola milioni 845) na John Boyega (dola milioni 815).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here