SHARE

NA SAADA SALIM

WAAMUZI wa Misri watachezesha mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga na Medeama FC ya Ghana, mchezo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), jana lilitaja majina ya waamuzi hao ambao ni Ibrahim Nour El Din ambaye atakuwa kati akisaidiwa na Ayman Degaish na samir Gamal Saad.

Mchezo huo ni muhimu kwa upande wa Yanga inayoendelea na mazoez Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi Hoteli ya Lugger Plazza, iliyoko Kunduchi kujiandaa na mchezo huo.

Katika hatua nyingine wapinzani wa Yanga kwenye michuano hiyo timu ya Medeama FC inatarajia kuwasili nchini kesho Alhamisi kwa ajili ya mechi hiyo.

Kocha wa timu hiyo, Prince Owussu, alisema msafara wa timu hiyo utawasili nchini Tanzania hiyo kesho lakini yeye atataja kikosi rasmi kitakachokuja leo Jumatano.

Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Madeama baada ya kupoteza mechi mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mechi zote, na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam  Juni 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here