SHARE

NA WINFRIDA MTOI

WACHEZAJI wanne wa Coastal Union, wamesimamishwa kwa madai ya kushawishi mgomo katika kikosi hicho kutokana na kutolipwa mshahara kwa muda mrefu.

Nyota wanaodaiwa kulimwa barua ni Haji Ugando, Hassan Hamisi, Prosper Mushi na Omary Salum.

Taarifa ambazo DIMBA imezipata kutoka ndani ya timu hiyo, zinasema hata mchezo wa Mtibwa Sugar walikuwa tayari wameandaliwa wachezaji wa kikosi cha pili kucheza.

“Kuna wachezaji wa Coastal Union wamesimamishwa muda mrefu hata kabla serikali kutoa tamko la kusimamisha Ligi Kuu Bara, kutokana na kuanzisha mgomo,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kupata taarifa hiyo, DIMBA lilimtafuta, kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda, ambaye alidai kuwa yeye hafahamu suala hilo labda watafutwe viongozi.

“Sijui kama kuna wachezaji wamesimamishwa, mimi kazi yangu ni kufundisha, watafute viongozi kama mwenyekiti anaweza kuzungumzia,” alisema Mgunda.

DIMBA lilitafuta Mwenyekiti wa klabu hiyo, Steven Mguto, lakini simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here