Home Habari WACHEZAJI SIMBA WAOGELEA MINOTI

WACHEZAJI SIMBA WAOGELEA MINOTI

897
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU


WACHEZAJI wote wa Simba wanaopata nafasi ya kuvaa jezi na kuingia uwanjani kucheza ndio wanaoshikilia utajiri ndani ya timu hiyo na hasa endapo watafanikiwa kushinda mechi ambapo hupewa kifuta jasho cha kuanzia shilingi laki nne kama motisha.

Mashabiki na wanachama wa Simba wamekuwa na kawaida ya kuchanga pesa kiasi cha kuanzia shilingi milioni 10 na kuendelea kwa ajili ya kuwapa bonasi wachezaji katika kila mechi, ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana hao waweze kupata matokeo mazuri katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Simba imeanzisha desturi hiyo mara baada ya kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo wadau mbalimbali wamekuwa wakijichangisha kiasi cha shilingi milioni 5, huku mwanachama na mfadhili wa timu hiyo, bilionea Mohammed Dewji (MO) akiongeza milioni 5 kwa ajili ya hamasa hiyo.

Katika kiasi hicho cha fedha zinazotolewa na wadau hao, wanaocheza uwanjani hupewa kiasi cha shilingi laki nne (400,000) kila mmoja na wale wanaovaa jezi na kukaa benchi kila mmoja hupata shilingi laki mbili (200,000).

Kwa upande wa wachezaji wasiocheza na wanaokaa jukwaani, wao huambulia kitita cha shilingi laki moja kila mmoja kama kifuta jasho.

Meneja wa Simba, Mussa Mgosi, alisema huu ni wakati wa wachezaji wa Simba kucheza kwa kujitoa endapo wana nia ya kutengeneza pesa ambazo zipo wazi kutoka kwa viongozi na wadau wao.

“Kila mtu afanye kazi kulingana na nafasi yake, wachezaji wajitume na wapambane kupata ushindi kama kweli wanahitaji kutengeneza pesa, viongozi nao wanafanya majukumu yao kwa nafasi zao, watu wanachanga pesa ambazo ni kama motisha kwa wachezaji,” alisema Mgosi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here