SHARE

NA MWANDISHI WETU,

YANGA waliwasili jana kutoka Moroni kisiwani Comoro, walikokwenda kukipiga na Ngaya de Mbe ya huko katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Timu hiyo iliwasili jana mida ya saa sita kasoro na kupokelewa na mashabiki kibao waliokuwa wakiwasubiri.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuwasili, wachezaji wawili wa Yanga ambao ni manahodha, Nadir Haroub Cannavaro na Haruna Niyonzima pamoja na kocha Msaidizi, Juma Mwambusi, walikwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kitengo cha Moi kwa ajili ya kumsalimia kigogo mmoja wa Yanga ambaye ni mtu muhimu ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, habari zinasema pamoja na wachezaji hao kwenda Muhimbili, lakini uongozi wa hospitali uliwazuia kumwona kigogo huyo kwa madai kwamba haikuwa sahihi wao kufanya hivyo muda huo.

Hadi wakati DIMBA Jumatano linakwenda mitamboni, haikufahamika kigogo huyo ni nani na iwapo walifanikiwa kumuona ama la.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here