SHARE

Karibuni wapenzi wa safu hii ya Mahusiano ya kimapenzi, naweza kuita kona hii ulimwengu wa mahaba.Nimatumaini yangu mtajifunza mengi na kuwa bora kwa wapenzi wenu.

WAKWE WANAWEZA KUVUNJA NDOA YAKO.

Nini maana ya mkwe? Mkwe ni mzazi wa mume au mke! Anaweza kuwa baba au mama! Lakini mkwe pia anaweza kuwa mtu aliyemlea mume au mke hadi alipokutana na mwenza wake na kukubaliana kisheria kuungana kuwa mke na mume. Hivyo basi, mkwe ni mzazi wako, hasa linapokuja suala la kuoana, na siku zote katika maandiko ya dini zote wanatufundisha kuwaheshimu wazazi wa pande mbili, ikiwa ni maana ya mkwe (mzazi wa sweetie wako) na mzazi wako waliofanikiwa kuwaleta duniani kwa uwezo wa Mungu!.

Wazazi wetu hawa ni muhimili mzuri sana katika ndoa zetu endapo watakuwa wenye nidhamu na upendo wa pande mbili, mtoto wake na mtoto wa mwenzake. Wakati mwingine wanaweza kuwa nguzo bora za mafanikio katika maisha yetu ya kila siku. Wapo wanandoa ambao waliweza kusaidiwa na upande wa wazazi wa mke au mume wakawa na maisha mazuri sana ya kujivunia. Lakini pia, wapo wazazi ambao ni mwiba kwa ndoa za watoto wao, kwa kuvuruga kila kitu kwasababu eti wao ni wazazi na wanauchungu na watoto wao bila sababu ya msingi.

Lakini wale wanaoishi vema na wazazi wao wa pande mbili, ni furaha na hadi leo wanaposikia mkwe wanakuwa na furaha sana na kuwaheshimu. Hii inatokana na malezi pia ya hao wazazi, maana usipokuwa mzazi bora utakuwa mkwe mbaya baadaye. Hivyo, nashauri ndugu msomaji, kabla ya kuoa..hebu jaribu kumchunguza au kufunua mafai ya maisha ya mwanaume anayetaka kukuoa au mwanamke unayetaka kumuoa, wazazi wake wanaishije? Ni kosa kubwa kukurupuka kuoa au kuolewa bila kujua familia za wazazi wa huyu mchumba wako.

Maana zipo familia zingine, ukiangalia kuanzia mama yake, haishi na mume na amekuwa ni wa kuachika tu kila anapoolewa, au baba mwingine ni mtu wa kuoa na kuacha, sasa inawezekana hata mtoto akawa ameiga maisha ya wazazi wake. Hivyo unajikuta unaingia katika majuto ya kusumbuliwa na mke au mume aliyepata malezi mabovu kutoka kwa wazazi.

Mfano: Hivi kama unaoa mwanamke aliyelelewa na mzazi ambaye enzi za usichana wake alikuwa akijiuza kimwili, unadhani unaweza kujenga mbegu gani? Lazima tu kutakuwa na tatizo katika ndoa yako, labda awe amelelewa na waumini wa dini wanaomjua Mungu.

Wanandoa wengine tangu kuolewa au kuoa, wamekuwa wakiteseka katika ndoa zao kwasababu tu ya vitendo vichafu vya wakwe. Wengine ndoa zimevunjika, kisa Mama mkwe au Baba mkwe! Zipo njia za kuishi nao! Nitaziweka bayana!

TABIA MBAYA ZA WAKWE!

Katika karne hii ya 21, ni ujinga kuona wakwe wanajaribu kuendesha maisha ya watoto wao wakati tayari ni watu wazima na wanafamilia zao bora. Wakwe wengine wamekuwa na tabia za kupanga hata bajeti za familia za watoto wao, aidha wakiume au kike na kuleta ugomvi.

Mara nyingi, unaona mama mkwe anakuwa akimfundisha mwanaye wa kike namna ya kumkalia mumewe. Ni ajabu kabisa, wapo pia wanaojaribu hata kuwapeleka kwa Sangoma eti waweze kuwashika nyota na kuwaendesha wanaume zao. Huu ni ulimbukeni! Kwanini usimjue Mungu?, mpaka unampeleka mwanao kwa waganga wa kienyeji? Eti amtulize mumewe asitamani vimada! Ha! Ha! Ha! Haipendezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here