Home Burudani Waliowahi kutoka na Rihanna waachia ngoma

Waliowahi kutoka na Rihanna waachia ngoma

2284
0
SHARE

LOS ANGELES, Marekani

NDIYO, washikaji wawili ambao ni wasanii wakubwa kwenye soko la muziki, Drake na Chris Brown, juzi walitambulisha kolabu yao inayoitwa No Guidance.

Drake mwenye umri wa miaka 32, na Brown (30), waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki anayekimbiza kwa mkwanja kwa upande wa wanawake, Rihanna.

Mwaka 2012, waliripotiwa kuzichapa katika klabu moja ya usiku, ikisemekana kuwa sababu kubwa ilikuwa ni bibiye huyo.

Lakini, kwa sasa wakali hao ni maswahiba wakubwa, ikifikia hatua ya kuingia studio kupika wimbo uliotoka Ijumaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here