Home Habari WANACHAMA MPIRA PESA WATAKA KUZICHAPA

WANACHAMA MPIRA PESA WATAKA KUZICHAPA

587
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

SIKU moja kabla ya Simba kushuka dimbani dhidi ya Azam, Wanachama wa Simba, Tawi la Mpira Pesa yenye maskani yake Magomeni Mikumi wameazisha vurugu hadi kufikia hatua ya kutaka kupigana.

Taarifa za uhakika kutoka kwa Mwenyekiti wa Tawi hilo, Ostadhi Masudi amethibitisha kutokea kwa vurugu hiyo hadi wanachama kutaka kushikana kutokana na kugoma kuhama katika jengo ambalo wamepanga kuweka ofisi zao.

“Tatizo kubwa ni tuliambiwa tuhame hapa muda mrefu lakini wanachama waligoma, imefikia hatua ya mwenye nyumba kunipeleka kwa Mtendaji wa Kata kunishtaki hivyo tuliambiwa tuhamishe vitu, hatua hiyo imesababisha wanchama kuanzisha vurugu,” alisema.

Ostadhi Masudi alisema chanzo cha ugomvi huo ni baadhi ya wanachama kugomea kuhama hapa, hata hivyo wamepewa notisi hadi Jumanne ya wiki ijayo wawe wameshahama katika mjengo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here