Home Habari WANAOTAKA UONGOZI SIMBA WAFIKIA 10

WANAOTAKA UONGOZI SIMBA WAFIKIA 10

1161
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE


WANACHAMA 10 wa Simba wamejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndilo lililotoa maagizo kwa Simba kufanya Uchaguzi Mkuu, baada ya uongozi ulioingia madarakani Juni 30, mwaka 2014 chini ya Rais Evans Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ëKaburuí kumaliza muda wao.

Makamu Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba ambaye ndiye Msemaji Mkuu wa kamati hiyo, Stephen Ally, aliliambia Dimba kuwa, mpaka kufikia jana walijitokeza wanachama 10 kuchukua fomu za kugombea uongozi katika klabu hiyo.

ìMchakato unakwenda vizuri mpaka sasa, (jana) ni wanachama 10 tu waliochukua fomu, japo siwezi kuwataja majina kwa kuwa tulikubaliana kutaja majina yote, baada ya mchakato mzima kumalizika siku ya kesho, hivyo nawaomba kuweni na subiraî alisema Ally.

Licha ya kwamba hakutaka kutaja majina hayo, taarifa kutoka Simba zinadai kuwa, Kaimu Rais, Salum Abdallah ëTry Againí, huenda akajitosa kuwania nafasi hiyo, lakini Iddy Kajuna ambaye ni kaimu makamu wa Rais ikisemekana ameshachukua fomu.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni ile ya Rais pamoja na wajumbe watano watakaoingia kwenye bodi ya klabu hiyo, huku mwekezaji ambaye ni Mohamed Dewji ëMoí naye akiwa na watu wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here