SHARE
Wema Sepetu

NA KYALAA SEHEYE,

MALKIA wa filamu na mrembo wa taji la ‘Miss Tanzania’ (2006), Wema Sepetu, amesema atawaumbua mashoga zake wote wenye tabia za kinafiki watakaojaribu kumsogolea kwani ameshawabaini kwa yale wanayomsema.

Wema ameliambia DIMBA kwamba, baadhi ya mashoga zake wa karibu wamekuwa wakimchafua kwa kusema kwa sasa hana lolote na amefulia kiuchumi.

Alisema ameamua kukaa kimya bila kuwajibu ili kujipa muda wa kutafakari yaliyomtokea mwaka uliopita kwani amepitia mambo mengi magumu ingawa watu wanajidanganya kwamba amefulia wakati hakuna ukweli.

“Sijafulia na anayefikiria hivyo imekula kwake, natafakari niliyopitia wanafiki nimeshawajua na mwaka huu atakayenisogelea sitaacha kumpasulia ukweli kwani kuna watu wamekuwa wakinitumia kama daraja la kupatia ustaa,” alisema Wema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here