SHARE

LONDON, England

MASHABIKI wa Arsenal walishindwa kuzuia hisia zao na kuanza kuzomea wakati klabu yao ikichapwa bao 4-1 na Liverpool kwenye mchezo wa kwanza wa Premier League, uliopigwa katika dimba la Emirates.

Hii ni mara ya pili kwa Arsenal kuanza ligi kwa kichapo, hali iliyowakasirisha mashabiki wa Arsenal walioanza kumzomea kocha wao, Arsene Wenger, kwa kushindwa kufanya usajili.

Lakini baada ya zomea zomea hiyo, Wenger aliibuka na kuonyesha kukerwa na mashabiki wake kwa kitendo cha kuzomea wachezaji.
Wenger alisema wachezaji wake walifanya kazi kubwa kwenye pambano hilo na walistahili pongezi.

“Niliona na kweli sikufurahishwa na kitendo kile, inatokea kwenye soka matokeo kama yale na mara nyingi tumeshaonyesha huwa tuna nguvu ya kutengua matokeo tukipata sapoti ya mashabiki wetu,” alisema Wenger.

“Kuwa nyuma kwa bao 4-1 kwenye uwanja wa nyumbani ni jambo gumu kwa aina ya vijana tulionao kwenye kikosi. Eneo letu la ulinzi halikuwa vizuri tangu mwanzo wa mchezo na wote tunafahamu kuwa ni majeruhi.

“Tunatakiwa kuuchambua mchezo na si kukasirika. Nimeshazoea hali hii kwa kuwa siku zote mashabiki huwa wanahitaji kushinda kila mchezo.”

Naye gwiji wa klabu hiyo, Thiery Henry, amemtupia lawama Wenger kwa sera mbovu za usajili anazoziendeleza na kutaja kama ni sababu kuu inayopelekea kuboronga kwa timu hiyo.
Mpaka sasa Wenger amefanya usajili wa wachezaji watatu tu, huku jina kubwa likiwa ni kiungo Granit Xhaka, waliyemtoa katika klabu ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani kwa ada ya pauni mil 34.

“Kitu pekee ambacho sikielewi ni vile tunavyoambiwa kuwa Arsenal ni klabu tajiri, tuna hela ya kugombea mchezaji yoyote sokoni,” alisema Wenger.

“Lakini mpaka msimu umeanza hatukuweza kupambana na yeyote sokoni. Sasa sielewi ukweli ni upi.

“Hivi Arsenal bado ni chaguo la kwanza kwa wachezaji kwa England? Kama mchezaji mkubwa akiwa sokoni, wana uwezo wa kupambana kumchukua?

“Sote tunajua kuwa pesa inaharibu sana soka, lakini nani anajali? Tunatakiwa kwenda sawa na mazingira.
“Lakini wachezaji wanaitaka Arsenal? Hili ni jambo la msingi sana ambalo tunapaswa kulizingatia. Sidhani kama sisi ni namba moja tena kwa England.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here