Home Michezo kitaifa Wenger bahili? Sikia kufuru aliyoifanya kwa Aubameyang

Wenger bahili? Sikia kufuru aliyoifanya kwa Aubameyang

553
0
SHARE
Pierre-Emerick Aubameyang

DORTMUND, Ujerumani

IMEBAINIKA kuwa Borussia Dortmund waliipiga chini ofa ya pauni mil 80 iliyotolewa na Arsenal kwa ajili ya straika Pierre-Emerick Aubameyang.

Taarifa hii imetolewa na wakala wa mchezaji huyo, Vincenzo Morabito, akisema kuwa Arsenal walitoa kiasi hicho mwanzoni mwa msimu huu, lakini ilishindikana baada ya Aubameyang kugoma kuondoka Dortmund.

Straika huyu wa kimataifa kutoka Gabon alifunga mabao 39 msimu uliopita na aliwahi kukaririwa akisema kuwa, kama akitaka kuondoka Dortmund basi klabu pekee atakayoichagua ni Real Madrid.

Morabito amedokeza pia mbali na Arsenal, klabu nyingine iliyokuwa ikimhitaji straika huyo ni Napoli ya Italia, ambayo ilikuwa na shida ya kuziba pengo lililoachwa na Gonzalo Higuain, aliyetimkia Juventus kwa kitita cha pauni mil 76.

“Kipindi cha nyuma kidogo nilimpigia Michael Zorc, Mkurugenzi wa Ufundi pale Dortmund, nilizungumza naye kuhusu uwezekano wa kufanya biashara ya Aubameyang baada ya kufanya mazungumzo na Napoli, lakini aliniambia haiwezekani.

“Najua pia mwanzoni mwa msimu Arsenal walitoa ofa ya pauni mil 80 kwa ajili ya Aubameyang, lakini uongozi ukagoma kabisa kuongelea habari hizo.”

Mchezo wa mwisho wa Bundesliga, Aubameyang alifunga mabao manne kwenye ushindi wa mabao 5-2 Dortmund walioupata dhidi ya Hamburg na kufikisha idadi ya mabao 14 kwenye michezo 14 aliyocheza mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here