SHARE

MUNICH, Ujerumani

SIKU yoyote kuanzia sasa, kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, atakutana mezani na mabosi wa Bayern Munich, ajenda ikiwa ni kuangalia uwezekano wa kupewa kazi ya kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo lililoachwa na Niko Kovac.

Kovac alifukuzwa baada ya Bayern kuchezea kichapo cha ‘mbwa koko’ cha mabao 5-1 kutoka kwa Eintracht Frankfurt na Wenger alisema yuko tayari kwenda kukalia kiti chake.

Akizungumzia uwezekano wa kwenda Bayern, Wenger alikiri kupigiwa simu na kigogo wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge, akisema walizungumza kwa muda mfupi.

“Tulikubaliana tutazungumza vizuri wiki ijayo kwa sababu kwa sasa niko mjini Doha (Qatar) hadi Jumapili usiku (leo). Hii ni kweli kabisa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here