SHARE

NA NYEMO MALECELA

YANGA wanatarajia kutua Mwanza hii leo tayari kuanza kambi kwa ajali ya maandalizi ya michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Bara, lakini wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wanaonekana kuwa tofauti kidogo.

Kinachotokea ni kwamba, licha ya ziara hiyo kuandaliwa na wadau wa klabu hiyo mjini Mwanza, ni kama vile imeamsha ari kwao na sasa wameamua kuwa karibu na timu yao katika kila hatua.

Wakiongea na DIMBA Jumatano kwa nyakati tofauti, mashabiki wa Yanga wanasema watahakikisha wanaifuatilia katika kipindi chote itakapokuwa kambini, lakini hata katika mechi itakayocheza iwe ya ligi au ya kimataifa ili mradi iwe inaihusu timu yao.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kile wanachokiona kuitenga timu yao na hivyo kuonekana kama vile nguvu ya mashabiki kukuwepo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tunapaswa sasa kusimama kidete na timu iwe jua au mvua hii ni Yanga yetu tukisema tutegeane hakuna kitakachofanyika,” alisema Said Rajab Magessa aliyejitambulisha kama mwenyekiti wa tawi la Yanga.

Kimsingi Wanayanga wengi karibu kila kona bado wanafikiria kichapo walichokipata cha bao 1-0 katika mchezo wa fungua dimba dhidi ya Ruvu Shooting, licha ya kufanya usajili wa kishindo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here