SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongomovie Jackline Wolper ameipa kisogo sikukuu ya wapendanao ‘Valentine Day’ na badala yake amesema kwa sasa yupo bize kutangaza biashara zake.
Wakati sikukuu hiyo ikitarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa juma hili mrembo huyo amesema kwake kila siku ni ya mapenzi na hana sababu ya kupa siku maalumu.
“Kwangu mapenzi yapo kila siku, hii ni siku tu kama siku nyingine, kuna watu wanaitumia vizuri lakini kuna wale ambao wameacha kabisa majukumu yao na kuifungia kazi siku hiyo,kwangu ni tofauti kidogo,kwanza sasahivi nipo bize na kutangaza bidhaa zangu za vitambaa katika duka langu”alisema Wolper.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here