Home Michezo Kimataifa YA COSTA YAMKUTA GIROUD

YA COSTA YAMKUTA GIROUD

0
SHARE

LONDON, England

BAADA ya Diego Costa kuambiwa wazi kuwa hayupo kwenye mipango ya kocha wake, mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud yamemkuta, baada ya kocha Arsene Wenger kumfungukia wazi kwamba hayupo kwenye mipango yake.

Kwa mujibu wa mtandao wa Metro, Wenger kwa sasa anatafuta straika mkali kwa ajili ya msimu ujao na Giroud huenda akawa chambo kwenye mpango wa Wenger wa kuvuta mshambuliaji mwingine, ama Kylian Mbappe au Alexandre Lacazette.

Pia, mtandao wa L’Equipe ulidai kuwa, Giroud amepewa ruhusa ya kuondoka Emirates na sehemu ya kwanza anayotarajiwa kutua Mfaransa huyo mwenye thamani ya pauni milioni 20 ni kati ya Lyon au Marseille.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here