Home Burudani YAMOTO BAND WAJIVUNIA ZIARA YA BARANI ULAYA

YAMOTO BAND WAJIVUNIA ZIARA YA BARANI ULAYA

528
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

KUNDI la muziki wa kizazi kipya nchini, Yamoto Band, limesema ziara yake yao barani Ulaya imewafungua macho kutokana na kuvuna vitu vipya ambavyo watatumia kuongeza ujuzi katika sanaa yao.

Mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Mbwana Yusuph, amesema wamefanikiwa kukutana na wasanii wengine wakati wa ziara yao hiyo na kujifunza mambo mbalimbali ambayo kwao yalikuwa mapya.

“Hii ni mara ya kwanza kufanya shoo kwenye hizi nchi, tumejifunza mambo mengi sana katika kuhakikisha tunainua muziki wetu juu zaidi,” alisema Maromboso.

Alisema wamefanya ziara katika nchi tano ambazo ni Norway, Sweden, Uswisi, Denmark pamoja na Ujerumani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here