Home Habari Yanga bado yamuota Mkude

Yanga bado yamuota Mkude

502
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

LICHA ya klabu ya Simba kumalizana na kiungo wao Jonas Mkude kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, viongozi wa Yanga wameonekana bado wanamuota nyota huyo kwa ajili ya kukitumikia kikosi chao.

Mkude alikuwa akiwindwa na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na Simba, lakini mwekezaji wa timu hiyo Mohammed ‘MO’ Dewji aliwahakikishia mashabiki kwamba kiungo huyo ataendelea kuwatumikia.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ndiye aliyezua gumzo mitandaoni baada ya kumtangaza mchezaji huyo kwenye mitandao ya kijamii.

Mwakalebela aliweka picha ya kiungo huyo kupitia mtandao wa WhatsApp na akimtakia kiungo huyo sherehe njema ya Iddi na alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alidai ni jambo la kawaida kwasababu anawaweka wachezaji wengi.

“Nimemuweka kama wengine ninavyowaweka, mchezaji akiwa bora hata akiwa si wa timu yako si tatizo, nafahamu alikuwa kwenye mipango yetu na imetokea hatujafanikiwa kupata saini yake,” alisema Mwakalebela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here