SHARE

NA MAREGES NYAMAKA NA ASHA KIGUNDULA

TIMU ya Yanga ambayo hadi sasa imecheza mechi sita tu za Ligi Kuu na kuwa na viporo vitano ili kufikia mechi 11 kama zilivyo timu nyingine zinazocheza michuano hiyo, Ijumaa ijayo itaanza kucheza mechi zake zilizosalia.

Wanajangwani hao watacheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Alliance Novemba 29, kisha itapiga mwingine Desemba 2, dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Baada ya mechi zake mbili, Yanga na Simba zinatarajia kuendelea na ligi Januri 4, mwakani ambapo utakuwa ni mtanange wa wawili hao maarufu kama ëKariokoo Derbyí kutokana na kusimama kwa michano hiyo, kupisha michuano ya Cecafa inayotarajia kufanyika Uganda.

Katika kipindi chote cha mwezi mmoja jeshi la kocha Boniface Mkwasa, litakuwa likijifua vilivyo kwa ajili ya mtanange huo, lakini pia ligi kwa ujumla.

Mkwasa baada ya kukiongoza kikosi chake kuwatungua JKT Tanzania mabao 3-2 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, aliwambia waandishi wa habari kuwa anatoa siku tatu pekee za mapumziko.

ìBaada ya mchezo huu tunatoa mapumziko ya siku tatu, Jumanne tunaanza mazoezi na kwa vile tutakuwa na muda mrefu wa kufanya mazoezi, tutajaribu kurekibisha mapungufu tuliyonayo, alisema.

Yanga ni timu pekee ambayo hadi sasa imecheza mechi chache zaidi (sita) na kufanikiwa kuvuna pointi 13 baada ya kupoteza moja dhidi ya Ruvu Shooting, sare moja mbele ya Polisi Tanzania na kutembeza vichapo kwa timu nyingine nne.

Akizungumzia hatua hiyo, Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) Boniface Wambura alisema kuwa, timu zenye mechi zilizosogezwa mbele au kuahirishwa zitacheza Novemba 29 na Desemba 2, baada ya michuano ya Chalenji iliyokuwa ianze Desemba mosi na sasa itaanza Desenba 7.

Alisema baada ya kuona michuano hiyo imesogezwa mbele bodi imepanga ratiba kwa mechi zote za viporo, ambapo Azam pia itakutana na JKT Tanzania Desemba 2 kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Wambura alisema kuwa timu ya Ndanda ambayo ilipata ajali ikiwa njiani kwenda mkoani Kagera nayo itacheza mechi yake ya kiporo dhidi ya Kagera Sugar Novemba 29 na kucheza mechi nyingine dhidi ya Biashara Desemba 2.

Alisema licha ya kuchezwa mechi hizo ratiba itaendelea kwa mechi nyingine za ligi hadi tareha ya kuanza kwa maandalizi ya michuano hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here