Home Michezo kitaifa YANGA KUONGEZA MAJEMBE 3

YANGA KUONGEZA MAJEMBE 3

8922
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba kikosi chao kitaongeza silaha tatu matata kwenye usajili wa dirisha dogo, hiyo ikimaanisha kuwa mzunguko wa pili wapinzani wao watapata tabu sana.

Akizungumza na DIMBA Jumatano jana kwenye ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Kijiweni, kocha mkuu wa Wanajangwani hao, Mwinyi Zahera, alisema mpaka sasa tayari wachezaji wawili wameingia kwenye anga zake.

Alisema kati ya wachezaji hao watatu, wawili watatoka nje ya nchi ambao tayari ana mawasiliano nao huku mmoja akitoka hapahapa nchini.

“Nadhani kwenye usajili huo nitaongeza wachezaji watatu, mmoja nafasi ya ulinzi, mwingine kiungo na wa tatu nafasi ya ushambuliaji.

“Tayari ninayo majina mawili ya wachezaji kutoka Kongo, ambapo mmojawapo anacheza soka la kulipwa nchini Gabon, huyu mkataba wake unamalizika Novemba, nadhani tutakuwa kwenye nafasi nzuri kumsajili,” alisema.

Kuhusu atakaowatema, Zahera alisema anatarajia kupiga panga wachezaji saba ambao anaona hawana msaada sana kwenye timu hiyo kwani lengo lake ni kuhakikisha wanarudisha heshima ya klabu hiyo kuendelea kutwaa makombe kama kawaida yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here