Home Habari YANGA MMEMSIKIA MKUDE LAKINI?

YANGA MMEMSIKIA MKUDE LAKINI?

1896
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE,

ZIKIWA zimebaki saa 72 kabla ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga kukutana, nahodha wa timu ya Simba, Jonas Mkude, amesema hakuna wa kuwazuia kuchukua pointi tatu kwa wapinzani wao siku hiyo.

Timu hizo zinakutana Jumamosi Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa 99 tangu waanze kukutana kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mkude alisema,wamejiandaa vya kutosha kuikabili kuelekea kwenye mchezo huo, baada ya kuvuna matunda ya kutosha kupitia kambi ya Zanzibar.

“Tunajua wenzetu nao wamejiandaa, ila nataka kuwaambia tu kuwa sisi tumejiandaa zaidi katika mapambano ya kuwanyoosha wapinzani wetu Jumamosi ili kujiweka sawa na mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here