Home Habari YANGA NAO LEO VEPEE?

YANGA NAO LEO VEPEE?

1176
0
SHARE
NA EZEKIEL TENDWA

YANGA wanachekelea Simba kufungwa na Green Warriors na kutupwa nje ya michuano ya Azam Sports Federation Cup, lakini wenyewe wameshtuka kwamba hizi timu ndogo zinakaza zinapokutana na timu kubwa na sasa Wanajangwani hao wamepania kuweka masihara pembeni watakapokutana na Reha FC.

Simba walijikuta wakifungwa jumla ya mabao 4-3, kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90, zikifungana bao 1-1 na kuvuliwa ubingwa wao na sasa Yanga wamejipanga kuingia na kasi ya ajabu nao wasije wakaaibishwa kama wenzao.

Yanga watacheza na Reha FC, huku kichwani mwao wakiwa na jambo moja muhimu  kuhakikisha wanashinda kwani lengo lao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na ubingwa huo wa Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA.

Licha ya kwamba kocha mkuu wa kikosi hicho, George Lwandamina, hayupo nchini lakini kikosi hicho kimesukwa vizuri na kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa na sasa kinasubiri tu kutoa dozi.

Lwandamina ameshindwa kufika kujiunga na kikosi chake kwa wakati kwani amefiwa na mtoto wake ambaye inasemekana alikunywa sumu nchini kwao Zambia.

Hata hivyo, mashabiki wa Yanga hawatakiwi kuwa na wasiwasi wowote juu ya kukosekana kwa kocha wao huyo kwani Nsajigwa amekuwa akiwanoa wachezaji wake na kuwafundisha mbinu mbalimbali kuelekea mchezo huo wa leo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here