Home Habari Yanga nayo ndani Ligi ya Mabingwa Afrika

Yanga nayo ndani Ligi ya Mabingwa Afrika

475
0
SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

KAMA ulidhani Simba pekee yake ndiyo itawakilisha Bara Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, basi maamuzi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) huenda yakakushutua.

Naam! Mabingwa wa zamani Ligi Kuu Bara, Yanga, nao watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao licha ya kumaliza nafasi ya pili wakiachwa pointi saba na watani zao Simba.

Hii ni baada ya taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikionyesha CAF kuthibitisha Tanzania Bara kuwa na timu nne katika mashindano ya kimataifa msimu wa 2019/20.

Taarifa hiyo ya CAF ilisema timu mbili zitashiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na zingine mbili katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nafasi hiyo imepatikana baada ya Tanzania kuwa katika nafasi ya 12 bora kwenye viwango vya ubora wa CAF.

Kufuatia ongezeko la timu, TFF kupitia taarifa iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo ilisema kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ambazo zimefanyiwa marekebisho na Kamati ya Utendaji baada ya kupatika nafasi nne, timu za Tanzania zitakazowakilisha katika mashindano hayo  ni Simba na Yanga huku Azam FC na KMC zikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kwa upande wa KMC watawakilisha Kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo ambaye inatamka kama timu iliyomaliza nafasi ya tatu itakua ndiyo bingwa wa Kombe la FA basi mshindi wan ne anapata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho kwasababu bingwa wa Kombe la FA anaiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo,” ilisema taarifa hiyo ya Ndimbo.

Taarifa hiyo iliongeza kusema tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu kupitia mtandao wa CMS na mwisho wa usajili ni Juni 30 mwaka huu ambapo TFF inatakiwa iwe imesajili timu zitakazoshiriki kwenye mashindano ya kimataifa msimu wa 2019/20.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here